Faida 5 za kuendesha Baiskeli

Miongoni mwa faida hizo ni;
1. Kuendesha baiskeli kunasaidia kupunguza kwa kiwango kikubwa mafuta mwilini, kwasababu hupunguza calori mwilini.
2. Baskeli ni usafiri rahisi unaoweza kujichanga ukanunua na ukaokoa bajeti ya nauli za kilasiku uendapo katika shughuli zako kama si mbali sana na maeneo unayoishi.
3. Hukufanya uwe karibu na watu wanaotembea kwa miguu, kwa mfano ukiwa njiani utasalimiana na watu mbalimbali, tofauti ilivyo gari.
4. Ukitumia baskeli hukupa nafasi ya kuona kupita sehemu ambazo kwa gari usingefika, hivyo hutumia njia fupi.
5. Kuendesha baiskeli husaidia kuimarisha misuli ya mwili hivyo kwa maneno mengine tunaweza tukasema licha ya baiskeli kutumika kama usafiri lakini vilevile ni chombo cha mazoezi, hivyo endesha baiskeli mara kwa mara ili kuuweka mwili wako sawa.