Mlima Kilimanjaro waingiza bilioni 471
Serikali
imesema hifadhi ya Mlima wa Kilimanjaro katika kipindi cha miaka kumi
kuanzia mwaka 2007 hadi 2017 imeingiza mapato ya Shilingi Bilioni 471
kupitia shughuli za utalii.
Mapato
hayo yameelezwa jana Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Japhet Hasunga wakati akijibu swali la Mbunge wa Vunjo, James
Mbatia aliyehoji mapato ya hifadhi ya mlima Kilimanjaro na matumizi
yake katika kipindi cha miaka kumi mfululizo.
Hasunga
alitaja matumizi ya mapato hayo, kwamba kiasi cha Sh. Bilioni 67.5
zilitumika kutengeneza miundombinu ya kuhifadhi mlima na Bilioni 46.6
kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za hifadhi katika kipindi cha miaka
kumi.
Pia,
alisema Bilioni 2.28 zimetumika katika utekelezaji wa miradi ya kijamii
kwenye vijiji vilivyo jirani na hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.