Tarime wateketeza mashamba ya bangi hekari 263. 5

Shamba la Bangi. 
Kamati
ya ulinzi na Usalama Wilayani Tarime Mkoani Mara kwa kuongozwa na Mkuu
wa Wilaya ya Tarime Glorious Luoga wameteketeza Mashamba ya Bangi yenye
hekari 263.5 Bangi Kavu Kg 210,Magunia yaliyokutwa majumbani 52 yenye
uzito wa kilo1560 na Mbegu Kg 75 huku wakikamatwa watuhumiwa 20.
Kamanda
wa Polisi Tarime Rorya SACP Henry Mwaibambe amesema kuwa zoezi hilo ni
endelevu huku Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usala Mkuu wa Wilaya ya
Tarime Glorious Luoga akitoa honyo kali na kusema wataendelea
kuwashughulikia wale wanaolima na kununua zao hilo haramu.

Wa pili kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime Luoga akiwa katika Shamba la Bangi


Zoezi la kufyeka linaendelea.
Bangi Kavu zikiwa kwenye magunia

Powered by Blogger.