Rais Magufuli hajatengua uteuzi wa Dkt. Laurian Ndumbaro
Taarifa
zinazoenezwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora Dkt. Laurian Ndumbaro sio za kweli na zipuuzwe.
Wananchi
endeleeni kupokea taarifa rasmi kutoka kwenye mamlaka na vyombo rasmi
vya Serikali, na pia watumiaji wa mitandao ya kijamii mnakumbushwa kuwa
kueneza taarifa za uongo ni makosa kisheria.
Serikali itawafuatilia wote waliozusha taarifa hizi na kuchukua hatua kwa mujibu wa sheria.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
