Picha katika Matukio tofauti Maadhimisho siku ya Wakulima na Wasindikaji wa zao la Muhogo yaliyofanyika Wilayani Rorya.

Mkuu
wa Wilaya ya Rorya Simon Chacha akiwa katika shamba darasa la zao la
Muhogo kijiji cha Nyamasanada kata ya Ikoma akionyesha mfano wa Muhogo
uliopandwa kwa kutumia mbolea ya samadi upande wa kushoto na ambao
haukutumia mbolea hiyo upande  wa kulia katika maadhimisho ya siku ya
Wakulima wa zao la Muhogo na wasindikaji wa zao hilo.

Maadhimisho
hayo yamefanyika katika kijiji cha Nyamasanda kata ya Ikoma Wilayani
Rorya Mkoani Mara kwa kushirikisha Wataalamu wa Kilimo na baadhi ya
Wakulima kutoka  Wilaya saba ambazo zinatekeleza mradi huo ikiwemo
Wilaya ya Serengeti, Rorya,  Bunda Magu, Biharamulo, Ngara na Sengerema
lengo ni kuongeza Mnyororo wa thamani katika uzalishaji wa Mbegu
zinazokinzana na magonjwa mbalimbali ili kukomboa Mkulima.

Katika
maadhimisho hayo wataalamu hao wameweza kutembelea shamba darasa pamoja
na kuangalia mashine inavyochakata Muhogo baada ya kutoka shambani.

Mkuu
wa Wilaya ya Rorya Simon Chacha akiongea na Wageni kutoka Idara
mbalimbali kabla ya Kwenda katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima wa zao
la Muhogo.



Rhoda
Mahava Mratibu wa Mradi wa kujenga na kuendeleza Mnyororo wa Thamani wa
zao la Muhogo  Kanda ya ziwa akitambulisha wageni alioambatana nao kwa
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Simon Chacha.
Rhoda
Mahava Mratibu wa Mradi wa kujenga na kuendeleza Mnyororo wa Thamani wa
zao la Muhogo  Kanda ya ziwa akifanya utambulisho katika maadhimisho
hayo.
Mkurugenzi
wa idara ya Sayansi  ya Chakula na Lishe Dr Elifatio  Towo akieleza
jinsi idara inavyofanya kazi katika kuboresha zao la Muhogo.
Wakuu wa Idara za Kilimo kutoka wilaya mbalimbali wakieleza mafanikio ya Mradi huo.
Afisa
kilimo Wilaya ya Rorya Dominick Ndyetabula akisisitiza kilimo cha zao
la Muhogo ambapo amesema kuwa kwa Rorya wanategemeza zao la Muhogo kwa
asilimia 30.
Afisa
Kilimo Mkoa wa Mara Denis Mgaya akieleza mikakati ya serikali ngazi ya
Mkoa katika kuboresha zao la Muhogo na upatikanaji wa Mbegu bora ambazo
zinakinzana na Magonjwa.
Mkuu
wa Wilaya ya Rorya Simon Chacha akihimiza zao la Muhogo huku akiwataka
vijana wajikite  katika kilimo na siyo kushinda Vijiweni, Mkuu wa Wilaya
amesema kuwa serikali ya Wilaya hiyo itaanza kutumia nguvu kubwa ili
vijana wakalime sasa, "Mfano ukipita sasa hivi kwenye vijiwe utakuta
vijana wanacheza karata wabibi na wazee ndo wako shambani lazima hili
kwa Rorya likomeshwe" alisema Mkuu wa Wilaya.



Wananchi pamoja na wakulima kutoka Wilaya saba zinazotekeleza Mradi huo wa kujenga na kuendeleza Mnyororo wa Thamani wa zao la Muhogo Kanda ya ziwa.

Wakielekea kuona Shamba Darasa la zao la Muhogo kijiji cha Nyamasanda kata ya Ikoma Wilaya ya Rorya Mkoani Mara.
Zao la Muhogo aina ya Mkombozi baada ya kuvunwa.
Meneja Mradi wa CAVA Nchini Tanzania  Grace Mahende  akieleza jinsi mradi unavyofanya kazi na kuendelea kuhimiza kilimo hicho.
Afisa Kilimo Mkoa wa Mara Denis Mgaya akionyesha wakulima ugonjwa unavyoshambulia zao la Muhogo.
Mkuu wa Wilaya ya Rorya Simon Chacha akitembelea shamba Darasa zao la Muhogo kijiji cha Masanda kata ya Ikoma.
Chenga za Muhogo ambao tayari umetolewa shambani na kuchakatwa na Mashine


Meneja
Mradi wa CAVA Nchini Tanzania Grace Mahende akieleza jinsi mashine ya
Kuchakata Muhogo inavyofanya kazi na kunufaisha wakulima hao.


Mshine ya kuchakata Muhogo unapotolewa shambani
Dr
Adebosola Opeodu Deputy Director kutoka Nchini Nigeria ambao ni
wafadhili wa Mradi huo akiongea na Wakulima ambapo amesema kuwa mradi
huo unatekelezwa Nchini Tanzania, Kenya, Malawi na Uganda lengo ni
kukomboa Mkulima.

Picha za Pamoja.Picha zote na CLEO24 NEWS.
TAZAMA VIDEO KUPATA HABARI KAMILI KATIKA MAADHIMISHO HAYO.
Powered by Blogger.