Kesi Mbili Zawasilishwa Mahakamani Kupinga Ushindi Wa Kenyatta
Kesi
mbili zimewasilishwa katika mahakama ya juu nchini Kenya, zikitaka
kufutwa kwa ushindi wa rais Uhuru Kenyatta kufuatia uchaguzi wa tarehe
26 mwezi Oktoba.
Kesi hizo ziliwasilisha mahakamani Jumatatu saa chache kabala ya siku ya mwisho.
Aliyekuwa
mbunge wa kilome Harun Mwau na mawakili Njonjo Mue na Khelef Khalifa,
wanasema kuwa katiba ilikiukwa wakati wa maandalizi ya uchaguzi huo.
Kesi
ya mwau ambayo inawashtaki IEBC, mwenyekiti wake na Rais Uhuru Kenyatta
ambaye alitangazwa mshindi kwenye uchaguzi wa mwezi Oktoba, inasema
kuwa kushindwa kwa IEBC kuruhusu vyama kuandaa uchaguzi wa vyama,
kuliwanyima wale ambao walitaka kugombea fursa ya kufaya hivyo.
Mwau
alijumuisha kipengee cha uamuzi wa mahakama, kuwa mgombea kwa chama cha
United Democratic Cyrus Jirongo alikuwa amefilisika kwa hivyo
hakustahili kuwania urais.
Kesi
iliyowasilishwa na mawakili Mue na Khalifa nayo kwa upande mwngine
ilizunguzia ukiukaji wa katiba ikiwemo kuchapisha picha za watu
wasiostahili kwenye makaratasi ya urais akiwemo mgombea wa muungano wa
NASA Raila Odinga, ambaye alikuwa ametangaza kuwa hangegombea urais.
Akiongea
na vyombo vya habari wakati wa kuandika kesi hiyo, wakili wa Mue na
Khalifa, Harun Ndubi, alisema kwa tume ya uchaguzi haukustahili kuandaa
uchaguzi kwa hivyo wanataka uchaguzi huo kuandaliwa upya.
Ndubi alisema kuwa tume ya uchaguzi ilikuwa na upendeleo kwa hivyo haikustahili kuandaa uchaguzi.
