KATAMBI KUHAMIA CCM...DR MASHINJI NA GODBLESS LEMA WATAKA WATANZANIA WATOFAUTISHE KATI YA WANAUME NA WAVULANA

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
amesema kwamba kisasi cha CCM kuchukua wanachama wake kitasaidia
kuwaondoa wavulana kwenye mapambano ya siasa za upinzani.
Lema ameyasema hayo ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa
Baraza la Vijana Chadema, Patrobas Katambi kuomba kuomba ridhaa ya
kuingia ndani ya Chama cha Mapinduzi leo katika kikao cha halmashauri
Taifa.
Lema amesema kwamba CCM imekuwa na kisasi kikubwa baada ya aliyekuwa
Waziri wa Maliasili mstaafu na Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro
Nyalandu kuondoka CCM
"Baada ya Lazaro kuondoka CCM , CCM wamekuwa na kisasi kikubwa , ambacho
kimsingi kitasaidia kuondoa wavulana ktk mapambano haya , bado Mameya
wawili ? Na kijana mwingine aliyekuwa shupavu 2010-2015. Msiogope kwani
wanawaogopa sana na ndio sababu ya matendo haya" Lema.
Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho
Dr. Vicent Mashinji amesema kwamba "Ni muda wa kutofautisha kati ya
wanaume na wavulana! wana CHADEMA msihofu tunazidi kuimarika. Kila
abiria atashuka kwenye kituo chake lakini safari ya ukombozi

