MZEE KANUMBA : HUKUMU YA LULU KWENDA JELA MIAKA MIWILI NI KAMA HUKUMU YA MWIZI WA KUKU
Saa chache baada ya mahakama kumhukumu
Mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ kwenda jela miaka miwili kutokana na
kifo cha Steven Kanumba,Baba wa marehemu Steven Kanumba mzee Charles
Kanumba ameibuka na kueleza kuwa hukumu hiyo haijamfurahisha
akifananisha hukumu hiyo kuwa kama hukumu ya mwizi wa kuku.
Akizungumza na Malunde1 blog,Mzee
Kanumba alisema hukumu hajaridhika nayo kwani hukumu ya miaka miwili ni
danganya toto kwa ndugu na wazazi hivyo ni bora wamuachie huru ijulikane
moja.
Alisema hukumu ya kwenda jela miaka
miwili haitoshi kwani anaifananisha na hukumu inayotolewa kwa wale
wanaoiba kuku siyo kwa yule aliyesababisha mtu kupoteza maisha hata kama
aliua bila kukusudia.
“Nimeipokea hukumu iliyotolewa na
mahakama..lakini hivi sasa sina cha kusema kwani tangu kesi ilipoanza
ilionekana kutotendeka haki mfano mtuhumiwa kuendelea kuwepo
Alisema kabla ya kutolewa hukumu hiyo
tarehe 13 Novemba mwaka huu aliiota ndotoni kuhusu hukumu ya kesi hiyo
na kuieleza familia yake kuwa yuko mahakamani na hakimu akiwepo Lulu na
mama yake mzazi na hukumu ilivyotolewa jana ni vile vile kama
alivyooteshwa lakini hajawahi kuwaona ana kwa ana watu hao.
“Mimi nasema kuwa sijawahi kumuona ana
kwa ana huyo binti anayeitwa Lulu na wala sijawahi kusikia sauti yake
kwenye simu hata mama yake mzazi simjui bali watu hawa huwa ninawaona
kupitia magazetini au kwenye televisheni tu basi”,alisema Mzee Kanumba.
Mzee Kanumba alisema marehemu Steven Kanumba alikuwa mwanaye wa sita na kifo chake kimeacha kubwa.
Na mwandishi wetu wa Malunde1 blog