Mwenyekiti wa baraza la Vijana Chadema (BAVICHA),Patrobas Katambi amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katambi ametangaza
kujiondoa Chadema leo Jumanne Novemba 21,2017 katika mkutano wa
halmashauri kuu ya CCM unaoendeshwa na mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
Dkt. John Pombe Magufuli jijini Dar es salaam.
Katambi alikuwa
mgombea ubunge jimbo la Shinyanga Mjini katika uchaguzi mkuu mwaka 2015
akikabiliana na Stephen Masele (CCM) ambaye aliibuka mshindi huku
Katambi akidai kuibiwa kura katika uchaguzi huo.
Mbali na Katambi makada wengine wa CHADEMA wameamua kurudi CCM. |