TUNDU LISSU APELEKWA KENYA KWA AJILI YA MATIBABU BAADA YA KUPIGWA RISASI
Tundu Lissu akipandishwa kwenye ndege
***
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu
ambaye ni mwanasheria mkuu wa CHADEMA na rais wa Chama cha Wanasheria
Tanganyika (TLS) amesafirishwa kwenda Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya
matibabu usiku wa kuamkia Ijumaa Septemba 8,2017 baada ya kupigwa risasi
akiwa Dodoma nchini Tanzania.
Ndege ya 5H-ETG iliyombeba Tundu Lissu
imetoka katika uwanja wa ndege Dodoma saa sita na robo kwa ajili ya
matibabu katika hospitali ya Agha Khan jijini Nairobi nchini Kenya.
Mbunge wa Rombo,Joseph Selasini amesema
katika safari hiyo Tundu Lissu ameambatana na mkewe,madaktari wawili
wasiokuwa na mipaka,mwenyekiti wa CHADEMA Taifa,Freeman Mbowe na Mbunge
wa Iringa Mchungaji Peter Msigwa.
Tundu Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana siku ya Alhamis Septemba 7,2017 akiwa kwenye gari lake nyumbani kwake Dodoma.
