BINTI ABAKWA HADI KUFA KINONDONI DAR ES SALAAM
Kundi la vijana wasiofahamika wamembaka
msichana wa miaka 20 hadi kufa na kisha kumtupa jalalani maeneo ya
jirani na nyumbani kwao Madale Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es
Salaam.
Wakisimulia tukuio wazazi wa binti huyo,
wamesema kuwa mpaka majira ya saa nne usiku kuamkia Jana Septemba 7
alikuwa nyumbani kabla ya kuwasili kwa vijana watatu waliokuja na
pikipiki (bodaboda) na kuanza kuzungumza naye kama marafiki kwa
takribani saa nzima na baadae binti yake kuaga akitaka kuwasindikiza na
hakurudi tena hadi alipopewa taarifa za kifo hicho.
Aidha Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa
Madale, Gration Mbelwa ameliomba Jeshi la Polisi kuhakikisha watuhumiwa
wanakamatwa na kuwaomba wanafamilia pamoja na rafiki za binti huyo kutoa
ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuwakamata watuhumiwa hao.