LOWASSA AMTEMBELEA TUNDU LISSU HOSPITALI YA AGA KHAN KENYA

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa yupo Nairobi nchini Kenya kumjulia
hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika
Hospitali ya Aga Khan, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu
wasiojulikana.
Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alijeruhiwa kwa risasi tano
Alhamisi Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini
Dodoma akitokea bungeni.
Katika akaunti yake ya Twitter, Lowassa ame-tweet akisema, “Earlier
today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS
and dear friend @tundulissutz He is recovering well. It is Sad times
for Tanzania. Let us all keep praying.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema “Mapema leo nilitembelea Hospitali ya
Nairobi kumwona mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika
(TLS) na rafiki kipenzi Tundu Lissu. Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha
masikitiko kwa Tanzania. Kwa pamoja tuendelee kuomba.”
Katika tweet hiyo, Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema,
ameweka picha akiwa pamoja na Alicia ambaye ni mke wa Lissu; Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe na dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.
