Sumaye: Sipo Tayari Kurudi CCM Kwa Mateso, Bora Waninyang'anye Kila Kitu
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CHADEMA ambaye pia ni Waziri Mkuu mstaafu, Frederick
Sumaye amefunguka na kusema licha ya mambo anayofanyiwa na serikali
ikiwa pamoja na kunyang'anywa mashamba yake lakini hawezi kurudi CCM.
Sumaye
amedai kuwa toka alipohama chama hicho na kuingia upinzani wapo
viongozi walitamka wazi kuwa dawa yake ni kupokonywa mali zake mpaka awe
masikini na kudai hayo mambo ndiyo yameanza lakini hayawezi kumfanya
kurudi tena katioka chama hicho.
"Hata
lile lililotokea Mwabepande nililitegemea kama mtakumbuka kipindi
nilichohama kutoka CCM na kuja upinzani mwaka 2015 katika kipindi cha
kampeni wapo viongozi walitamka wazi kuwa huyu dawa yake kunyang'anywa
mali zake mpaka awe masikini, nilipoanza kuandikiwa barua mara sijafanya
hiki sijui sijafanya hiki nikajua wazi kuwa hakuna sababu nyingine
zaidi ya sababu za kisiasa na nina adhibiwa kwa kuwa nimekwenda
upinzani" alisema Sumaye
Aidha
Sumaye amekiri kuwa mashamba hayo aliyapata kwa njia halali na siku
zote amekuwa akiyalipia kwa muda wote huo na kusema mashamba yake yeye
amekuwa akiyaendeleza tofauti na inavyoelezwa kuwa mashamba hayo
hayaendelezwi.
"Mimi
nitaiachia mahakama iendelee mpaka hapo itakaposema ama imeshindwa ama
nifanye nini kama wanafikiria mimi nitarudi CCM kwa kuteswa, nasema
sirudi CCM eti kwa sababu nateseka" alisisitiza Sumaye
Serikali
imetangaza kuchukua mashamba mbalimbali ya wananchi ambayo
hayajaendelezwa kwa muda mrefu na wamiliki wa waeneo hayo, jambo ambalo
limemkuta na Mhe. Sumaye kwa mashamba yake mawili kudaiwa kuchukuliwa na
serikali kwa kigezo hicho hicho kuwa hayajaendelezwa kwa muda mrefu.
