Rais Magufuli: Hakuna Hela ya Bure katika Utawala Wangu, Lazima Watu Wafanye Kazi
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefunguka
na kusema katika wakati wake hakuna kupata pesa kwa njia rahisi kwani
lazima ufanye kazi kweli ili kupata pesa halali.
Rais
Magufuli amesema hayo leo Handeni wakati anaelekea mkoani Tanga kwa
ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta
kutoka Hoima nchini Uganda mpaka Chongoleani Tanga. Utaofanyika siku ya
Jumamosi ya tarehe 05 Agusti mwaka huu.
"Kuna
watu walikuwa wamezoea vya bure wanapiga 'disco' tu wanapewa hela
nyingi hazipo pesa za namna hiyo, hivi sasa watu wanataka ufanye kazi
uzalishe mali ili upate fedha za kweli na asiyefanya kazi asile na
usipokula maana yake ufe" alisisitiza Rais Magufuli
Mbali
na hilo Rais Magufuli amesema uchumi wa Tanzania unakuwa kwa kasi kubwa
na kudai kwa Afrika katika nchi tano ambazo uchumi wake unakuwa kwa
kasi kubwa Tanzania pia ipo imeshika nafasi ya pili nyuma ya Ethiopia.
"Ikiwa
uchumi wetu unakuwa kwa asilimia 7.2% wapo watu watakuja na kulalamika
hela zimepotea, hao walikuwa wamezoea vya bure, na hao ndiyo mnawaona
wanapiga kelele" alisema Magufuli.
Kwa
mujibu wa benki ya Dunia katika nchi ambazo uchumi wake unakuwa kwa
kasi kubwa Tanzania imekuwa nafasi ya tano chini ya India, Nepal,
Uzbekistan na Ethiopia ambayo ndiyo imekamata nafasi ya tano.