MWENYEKITI WA YANGA TAWI LA KITUNDA, ANAWAKARIBISHA WANAYANGA ISHU YA MWALI WA LIGI KUU BARA KUTEMBEZWA
Mwenyekiti
wa Yanga Tawi la Kitunda jijini Dar es Salaam, Boaz Ikupilika
anawakaribisha wanafanya katika sherehe ya ubingwa wa 27 ukiwa pia ni wa
mara ya tatu mfulilizo.
Kombe
hilo la ubingwa wa Tanzania Bara tutalitembeza Kesho Jumapili mitaa ya
Ukonga na baadaye litafika tawini na pia wanachama wapya watapata fursa
ya kujisajili na benki ya posta na kukabidhiwa kadi zao.
Sherehe
zitaanzia tawi la Majumbasita kuanzia Saa 3:00 asubuhi na kupitia mitaa
ya Ukonga na kurudi njia ya banana mpaka kitunda na mitaa yake
Baadaye litarejea Majumbasita ambapo sherehe zitapambwa na burudani ya Msaga Sumu na shamrashamra nyingine kibao.
Karibuni sana.
Mimi mwenyekiti wa Tawi.
