MBUNGE MATIKO ACHANGIA UJENZI MSIKITI MKUU WA IJUMAA WILAYA YA TARIME NA KUTOA MSAADA WA VITABU VITAKATIFU VYA QURAN.
Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akikabidhi vitabu vya Dini kwa Viongozi wa Kiislam Wilayani Tarime Mkoani Mara. |
Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther N. Matiko akiendelea na Ziara
yake ya kutembelea makundi mbalimbali ya wananchi wake na kuzungumza nao kuhusu
Mustakabali wa Jimbo la Tarime Mjini katika kuwaletea wananchi wake Maendeleo,
Mhe Matiko amepata kufika ndani ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa Tarime na Kuzungumza
na Viongozi wakuu wa BAKWATA Wilaya ya Tarime. Ikiwa ni sehemu ya Maisha ya Mhe Matiko kuendelea kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika kumtolea Nazili kama alivyokwisha kufanya sehemu mbalimbali yakiwemo Makanisa tofauti tofauti, Mhe Matiko amepata kufanya hivyo ndani ya Msikiti Mkuu wa Ijumaa. Katika kuendelea kulitangaza Neno la Allah (Mungu) na kuwafanya watu wa Tarime waendelee kuishi katika Maandiko ya Vitabu Vitakatifu vilivyoo jaa Maarifa yote kuliko Vitabu vyote, Mbunge wa Tarime Mjini Mhe Esther N. Matiko ametoa Msaada wa Mabox Matatu yaliyo na jumla ya Quran 108. Mhe Esther N. Matiko _hakuishia katika Vitabu hivyo vya Allah ili Msikiti Mkuu wa Tarime upate kusonga mbele. Mhe Matiko ameweza pia kuchangia Mifuko 10 ya Saruji katika ujenzi wa Choo cha Msikiti huo baada ya kupata Ombi hilo kutoka kwa Viongozi wa Msikiti wa Ijumaa Tarime. Akizungumza mbele ya Mhe Matiko *Ostadh Nuruh Ismail,amemshukuru sana Mhe Matiko kwa msaada wa Quran hizo na Mifuko ya Saruji itakayosaidia kwa pamoja kuendelea kulitangaza neno la Mwenyezi Mungu kwa watu wa Tarime. Ostadhi Ismail amemuomba Mhe Matiko kuendelea kuwa nao bega kwa bega na hata kuwatafutia Wafadhili wengine watakaojitolea kama yeye jinsi alivyofanya. Katibu wa BAKWATA Wilaya ya Tarime naye hakusita kumkumbusha Mhe Matiko kuhakikisha anatimiza Ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo la Tarime Mjini ikiwemo ahadi ya ujenzi wa Maktaba. Lakini pia amemtia Moyo Mhe Matiko na kumuhakikisha ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Viongozi hao kwani ni Kiongozi wa mfano kupata kutokea Tarime Mjini. Kwa upande ewake Shehe mkuu wa Wilaya ya Tarime (BAKWATA) amesema kuwa hatua anazozichukua za kuzungumza na Makundi mbalimbali ndani ya Jimbo linaonehs moyo wa kazi. Shehe Mkuu wa Wilaya ya Tarime amempongeza zaidi Mhe Matiko baada ya kuchukua maamuzi ya kuzungumza na Viongozi wote wa Dini ndani ya Jimbo la Tarime Mjini mnamo 15/7/2017 ndani ya Ofisi ya Mhe Matiko iliyoko Mtaa wa Kebikiri Kata ya Turwa. Shehe Mkuu wa Wilaya ya Tarime* baada ya kupokea Misaada hiyo kutoka kwa Mhe Matiko amemshukuru sana na kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kumjalia Afya njema na Maarifa ya kuendelea kuwatumikia Wanatarime. Aidha Matiko ameshukuru Viongozi hao wa dini ya kiislamu Wilaya ya Tarime kwa ushauri mzuri waliompa kuhakikisha anatimiza Ahadi zake kwa Wanatarime Mjini kuanzia yale ya Serikali kuu na yale yaliyo ndani ya Halmashauri ya Mji wa Tarime. |