Madini yampaisha Rais John Magufuli
Wajumbe
wa kamati ya kuratibu rasilimali ya madini kwa nchi za Ukanda wa Maziwa
Makuu wamepongeza Rais Dk John Magufuli kwa jitihada anazofanya za
kudhibiti uvunaji haramu wa rasilimali hiyo na wamewaomba viongozi wa
nchi zingine kuiga mfano huo.
Wakizungumza
baada ya kumaliza kikao chao kilichokuwa kinafanyika mjini Arusha,
wajumbe hao kutoka nchi 12 za Ukanda wa Maziwa Makuu walishauri jitihada
zilizoonyeshwa na Rais John Magufuli zifanyike katika nchi zote za
ukanda huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha sheria zote za uchimbaji,
uuzaji wa madini zinazingatiwa na nchi husika zinanufaika.
Mratibu
wa kikao hicho kutoka sekretarieti ya nchi za ukanda huo, Balozi
Zachary Muhuri Muita, alishauri uchimbaji wa madini ufanyike kwa njia
halali na wachimbaji walipe kodi.