| Aliyekuwa mke wa rais wa Msumbiji, Samora Machel, Mama Graca Machel ambaye pia ni mwanzilishi wa Taasis ya Graca Machel Trust amewataka vijana kuweka mipango ya kujiletea mandeleo ya kiuchumi .
Mama Machel alisisitiza hayo Jumatano wiki hii alipokuwa akizungumza na vijana wa nchi mbalimbali jijini
Dar es salaam katika mjadala uliofanyika kujadili changamoto
zinazowakabili vijana wa Afrika katika hasa katika eneo la uchumi.
Mjadala huo ulikuwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana duniani ambayo imeadhimishwa leo Agosti 12 .
Graca Machel ambaye pia aliyekuwa mke wa rais wa kwanza wa Afrika Kusini, Nelson aliwataka vijana kuacha kulalamika na baadala wawe wabunifu.
|