DAWASCO YAANZA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI JUU YA MFUMO MPYA WA UTOAJI NA UPATIKANAJI WA TAARIFA MUHIMU
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi Everlasting Lyaro akitoa elimu juu ya
matumizi ya mfumo wa DAWASCO kwa kwa njia ya simu kwa watumiaji wa
vyombo vya Moto hususani Bajaj na Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya
Jiji la Dar es salaam. Mfumo huo umezinduliwa rasmi ili kutoa nafasi kwa
wananchi kupata na kutoa taarifa sahihi za DAWASCO.
Mmoja ya waendesha bodaboda akimuuliza swali Meneja Uhusiano wa DAWASCO,
Bi. Everlasting Lyaro juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWSCO katika
utoaji na upatikanaji wa taarifa.
Mwendesha bajaji akihojiwana ITV juu ya matumizi ya mfumo mpya wa DAWASCO katika utoaji na upatikanaji wa taarifa.
***
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Everlasting Lyaro, amewataka wananchi wa
Dar es Salaam na Pwani kupakua mfumo huu kwani ni rahisi kuutumia na
hauna gharama zozote. Anasema ni mfumo ambao utamrahisishia mteja kupata
taarifa muhimu zinazohusu huduma ya maji zikiwamo ankara ya mwezi,
taarifa za lini mteja alifungiwa huduma ya maji, muda ambao alifanya
malipo, lini mita yake ya maji ilisomwa na taarifa nyingine nyingi.
“Nawasihi wateja wetu na wananchi wote kupakua mfumo huu mpya katika
simu zenu za mkononi ili kuweza kufurahia huduma zetu, hakuna gharama
zozote ambazo utatozwa. Kupitia mfumo huu utaweza kupata taarifa zote
muhimu za huduma ya majisafi zikiwemo taarifa za mivujo ya maji na
ankara za maji za kila mwezi,”amefafanua Bi. Lyaro.
Amesema kwa sasa Wateja hawana haja ya kutumia muda mrefu katika
ufuatiliaji wa kuunganishwa huduma ya maji, bali kilichorahisishwa ni
mteja kuweka taarifa zake sahihi kwenye mfumo huo na DAWASCO.



