Waziri Mwakyembe Amtumbua Rasmi Malinzi.....Ni Baada ya Kusitisha Uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wote wa BMT
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) , Dionis Malinzi, ambaye ni ndugu na Rais wa Shirikisho la Soka Jamali Malinzi ametumbuliwa leo na Waziri wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt Mwakyembe kufuatia agizo la Waziri Mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimtaka Waziri Mwakyembe kupitia baraza hilo na kulitathimini hivyo baada ya kulipitia na kutathimini amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa baraza hilo.
"Kwa mamlaka niliyopewa na sheria ya BMT Na. 12 ya 1967, nimesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wote wa BMT" amesema Dkt.Harrison Mwakyembe
Kwa mujibu wa Waziri Mwakyembe amesema kuwa Sekretarieti ya Baraza la Michezo Tanzania litaendelea na kazi kwa kushirikiana na serikali wakati mchakato wa kuteua mwenyekiti mpya wa baraza hilo ukiendelea.