Waziri Mkuu awaonya madiwani Kyela.....Awapa siku mbili kumaliza tofauti zao, Vinginevyo Atalivunja Baraza Hilo
Serikali
imewapa siku mbili Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Mkoani
Mbeya kumaliza tofauti zao zinazokwamisha utendaji wa Halmashauri hiyo
na kuendelea kufanya kazi walizotumwa na wananchi.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Kassim Majaliwa jana Julai 29, 2017 wakati akizungumza na watumishi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Kyela akiwa katika ziara yake ya kikazi Mkoani
Mbeya.
“Baraza
la Madiwani limegawanyika,mnamgogoro tunataka uishe na mshirikiane na
mshikamane katika kufanya shughuli za maendeleo ili wananchi waweze
kupata manufaa. Mkiendeleza migongano hatutawavumilia Serikali inauwezo
wa tutalivunja baraza.”
Majaliwa
amesema ikifika Jumatatu Julai 31, 2017 Madiwani hao wawe wamemaliza
tofauti zao na wawaite wakuu wa Idara na kuwapa taarifa hiyo ili
shughuli za maendeleo ziendelee kutekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.
Tofauti
hizo ambazo zimedumu kwa takriban mwaka mmoja zimesababisha Madiwani
hao kushindwa kufanya vikao jambo linalokwamisha shughuli za maendeleo
ya wananchi katika Halmashauri hiyo.
Amesema
baadhi ya Madiwani hao wanawatetea watumishi waliosimamishwa kazi kwa
tuhuma za kuiibia Serikali mabilioni ya fedha jambo ambalo halikubaliki
na halivumiliki. “Naombeni mmalize tofauti zenu mara moja kabla
sijaondoka.”
Aidha,
Majaliwa ameiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU)
mkoa wa Mbeya kuhakikisha watumishi wote waliohusika katika kula fedha
za umma wanachukuliwa hatua kama alivyopendekeza Mkaguzi na Mdhibiti wa
Hesabu za Serikali(CAG).