Jeshi la Polisi Dar lakamata vifaa mbalimbali vya magari na Wezi 73
Jeshi
la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limewakamata watuhumiwa 73 wa
wizi wa magari pamoja na vifaa vya magari katika oparesheni yake maalum
inayolenga kuwakamata wezi na wanunuzi wa vifaa vya magari.
Taarifa
ya jeshi hilo, iliyotolewa jana na Kaimu kamanda wa Polisi kanda maalum
Dar es Salaam, (DCP) L. J Mkondya inaeleza kuwa tarehe 21/07/2017
walifanikiwa kuwakamata wezi wa vifaa mbalimbali vya magari, ikiwa ni
pamoja na wanunuzi wa vifaa hivyo katika sehemu mbalimbali za jiji la
Dar es Salaam.
Katika
Operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 73 wamekamatwa baada ya kupekuliwa
walikutwa na vifaa mbalimbali vya magari ikiwemo, Side mirrors, taa za
gari, bampas, left pump, milango ya magari, vitasa vya magari, power
windows, radio, injector pump, starer na seat cover.
Watuhumiwa
waliokamatwa katika mkoa wa kipolisi Kinondoni ni 29, Ilala 33 na Mkoa
wa kipolisi Temeke ni 11, watuhumiwa hao walishindwa kuvitolea maelezo
vifaa hivyo, na kuwa upelelezi bado unaendelea ili kubaini mtandao
unaojihusisha na wizi huo ambapo watafikishwa mahakami mara tuu
uchunguzi utakapo kamilika.
Kwa
ujumla vifaa vyote vilivyo kamatwa ni, Radio 12, Taa za magari aina
mbalimbali 105, side mirrors 92, vitasa vya gari 109, switch 7, Bampa 4,
Left Pump 3, Air Cleaner 1, Booster 3, Show grill, Mashine ya
kupandishia vioo 1 na Tyre used 2.