WALICHOTUPA SPORTPESA, EVERTON TUNASTAHILI KUSEMA AHSANTE PIA
Na Saleh Ally
KUNA
picha inasambaa katika mitandao mbalimbali ulimwenguni, wachezaji wa
Everton FC ya England wakiwa wameshika bango lililoandikwa “Asante
Tanzania”.
Kwa
mujibu wa mtandao wa mashabiki wa Everton, unaeleza kwamba kwa Ulaya
wanakadiria bango hilo limesomwa au kuonwa na zaidi ya mashabiki milioni
12 wa soka.
Pia
wanaamini bango hilo limeonekana kwa zaidi ya mashabiki milioni 18
duniani kote kwa wale wanaoweza kusoma Kingereza na Kiswahili pia. Bado
mtandao huo unaeleza bango hilo litakuwa limeonwa na zaidi ya watu
milioni 50, mwishoni mwa mwezi huu.
Wanaamini
hivyo kutokana na kasi kubwa ya maswali mengi ambayo wamekuwa wakipata
kutoka sehemu mbalimbali duniani kuhusiana na Tanzania na maana ya neno
Asante. Lakini pia taarifa wanazoelezwa na mashabiki wengi wa Everton
wakiwemo wale wa nchi za Bara la Asia na hasa Thailand.
Wakati
wa ujio wa Everton hapa nchini huenda ulionekana haukuwa na nguvu sana
hadi siku nne kabla ya safari ilipofanikiwa kumsajili Wayne Rooney
kutoka Manchester United.
Wakati
Everton imekuja hapa nchini, hakuna anayeweza kupinga kuwa nchi yetu
imejitangaza sana kupitia klabu hiyo hasa Wayne Rooney ambaye kwa sasa
ndiye mchezaji nyota zaidi kwa wale raia wa England.
Wakati
Everton wametutangaza na mwisho kumalizia kwa ujumbe mzuri wa “Asante
Tanzania”, hakika ni faraja kubwa lakini vizuri tuwape shukurani zao
waandaaji wa mechi hiyo, Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportPesa.
Tunakubali
wote kuwa tumejifunza mambo kupitia ziara hiyo na mambo hayo yanaweza
kuwa mazuri zaidi kama tutajifunza kupitia yale tuliyoyaona kabla ya
Everton kutua nchini, walipowasili na baada ya wao kuondoka.
Maandalizi:
SportPesa
walifanya maandalizi bora kabisa na kwa maana ya biashara huenda hata
makampuni ya hapa nyumbani au klabu zetu zingeweza kujifunza.
Mfano
angalia kwenye geti kuu la kuingilia wachezaji kwenda kwenye Uwanja wa
Taifa jijini Dar es Salaam. Utaona palipambwa kwa timu mbili za Everton
na Gor Mahia, kabla haikuwahi kufanyika hivyo. Hata kama si timu,
inaweza kutengenezwa picha nzuri inayohusu utalii wa Tanzania au
vinginevyo pamoja na bendera yetu ya taifa ikawa ya kudumu au kadhalika.
Basi:
Mara
zote tumeona timu zinakuja hapa na wanatumia magari ya kukodi
yanayobaki kama yalivyo. Angalia SportPesa walichokifanya kwa basi la
Shabiby. Hata kama walipata gharama lakini siku mbili basi hilo
lililotembea na wachezaji, walijitangaza kwa kiasi kikubwa.
Walikuja Brazil na timu kadhaa kabla. Hatukuwahi kuitumia nafasi kama hiyo na vema hilo likawa somo pia.
Hata wakati wakishuka kwenye ndege, ngazi zilikuwa na jina la Tanzania na pia nembo za SportPesa.
Mengi
yalikuwa mazuri ingawa mpangilio wa waandishi kuingia kidogo ulikuwa na
walakini na wanapaswa kuurekebisha wakati mwingine.
Wachezaji:
Wachezaji
wa Everton, licha ya kuwa na safari ndefu lakini walipata muda wa
kutembelea sehemu mbalimbali wakiwa katika makundi. Mfano kuwatembelea
albino, watoto wa Shule ya Msingi Uhuru, kukutana na Wamasai, kuweka
maua kama ishara ya heshima katika makaburi ya mashujaa na kadhalika.
Uwanjani:
Uwanjani, utaona mapango yalivyokuwa na mpangilio mzuri na hata mpangilio mzima wa mchezo.
Mechi
ilikuwa nzuri, imani yangu kama nilivyowahi kuandika awali, makipa
walijifunza kama ilivyo kwa mabeki kwa kuangalia mabeki wenzao, pia
viungo, washambulizi na hata makocha.
Hii
ndiyo maana ya kumkaribisha mgeni anayeweza kuacha somo bora lakini
kuwa na mwenyeji mtaalamu katika ukaribishaji mgeni na mwisho ni faida
hii. Ndiyo maana nikasema kwa kuwa wachezaji wa Everton wamesema “Asante
Tanzania”, nawaambia ahsanteni pia, nyie pamoja na wenyeji wenu.