MAYWEATHER ASIMAMISHA GARI USWAHILINI, APIGA SELFIE NA MASHABIKI
Baada ya kurejea kutoka kutangaza pambano lake dhidi ya Conor McGregor,
bondia Floyd Mayweather amesimamisha gari barabarani na kuwapa nafasi
mashabiki kupiga naye picha “selfie”.
Bondia huyo ambaye hajawahi kupigwa katika mapambano yake 49, alisimama
mbele ya mashabiki hao ambao hawakutegemea na kupiga naye picha.
Mayweather alisimama katika eneo la “Uswahilini” la Harlem na kuwapa mashabiki hao nafasi ya kupiga picha.