Wahalifu Wawili KIBITI Wauawa na Jeshi la Polisi
Jeshi
la Polisi nchini limefanikiwa kuwaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa
ni miongoni mwa wahalifu wanaoendesha mauaji katika Kanda maalumu ya
kipolisi Rufiji ambapo mmoja kati ya watu hao ametambulika kwa jina
la Abdallah Ally Ngande Makeo ambaye alikuwa anatafutwa na Jeshi la
Polisi kwa muda mrefu kutokana na kushiriki kwake katika matukio ya
mauaji maeneo ya Ikwiriri, Kibiti pamoja na uvamizi wa kituo cha Polisi
Ikwiriri.
Akielezea
tukio hilo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi, Naibu
Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas alisema kuwa tukio hilo lilitokea
mnamo tarehe 19, julai, 2017 saa mbili usiku katika eneo la Utende kata
ya Ikwiriri, wilaya Rufiji kanda maalum ya Polisi Rufiji.
“Askari
Polisi wa doria waliwatilia mashaka watu wanaokadiliwa kuwa watano
ambapo walipoanza kuwafutilia ndipo walianza kukimbia huku
wakiwashambulia askari kwa risasi.
"Askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.
"Askari nao kwa ujasiri walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi wahalifu wawili miongonio mwao ambao baadaye walifariki wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya muhimbili kutokana na kuvuja damu iliyosababisishwa na majeraha ya risasi waliyoyapata” alisema Sabas.
Aliongeza
kuwa katika eneo hilo la tukio ilipatikana silaha moja aina ya rifle
375 ambayo ilikutwa imekatwa kitako na mtutu ikiwa na risasi mbili
(2). Aidha, Miili ya marehemu wote wamehifadhiwa katika chumba cha
kuhifadhia maiti hospitali ya Taifa ya muhimbili.
Kamanda
sabas ameendelea kutoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na
Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa wahalifu
wengine waliosalia na kwamba opereheni hiyo ya kuwasaka wahalifu katika
Kanda hiyo ya kipolisi Rufiji ni endelevu na hakuna atakayebaki.