Tundu Lissu Agoma Kupima Mkojo....Polisi Waondoka na CD 6
Baada
ya jeshi la polisi kumkamata Tundu Lissu siku ya Alhamsi uwanja wa
ndege akiwa anaelekea nchini Rwanda. Jana jeshi hilo lilikwenda kufanya
upekuzi nyumbani kwa Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) ambaye pia ni
Mwanasheria Mkuu wa chama hicho.
Siku
ya jana Ijumaa ya tarehe 21/07/2017 jeshi la polisi walimchukua Tundu
Lissu na kwenda naye mpaka kwa Mkemia Mkuu wakiwa na lengo la kutaka
kumpima mkojo kabla ya kuelekea nyumbani kwake kufanya ukaguzi. Lakini
kiongozi huyo aligoma kufanya kipimo hicho kwa madai kuwa tuhuma
anazotuhiwa haziendani na vipimo hivyo.
Kwa
mujibu wa Tumaini Makene ambaye ni Afisa habari wa (CHADEMA) anasema
kuwa jana polisi baada ya kufanya ukaguzi nyumbani kwa Tundu Lissu
waliweza kuchukua CD 6 na kuondoka nazo.
"Jeshi
la Polisi bado linamshikilia, Mhe. Tundu Lissu, Kwenye upekuzi jana
nyumbani kwake walichukua CD 6 za 1996 zinazohusu masuala ya mgodi wa
Bulyag'hulu, Shinyanga" ilisema taarifa ya CHADEMA
Leo
ni siku ya pili toka kiongozi huyo anashikiliwa na jeshi la polisi Dar
es Salaam lakini Wakili Peter Kibatala pamoja na Wakili Fatma Karume wa
IMMA Advocates kwa upande wao wanasema wanaendelea na juhudi za kisheria
kuhakikisha kiongozi huyo anapatiwa dhamana au kufikishwa mahakamani
mapema iwezekanavyo.