Spika wa Bunge Job Ndugai achoshwa na wanaodhihaki bunge.

Spika
wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai amefunguka
kuwa wabunge wanaodai kuwa bunge ni dhaifu basi ni wazi watakuwa na
mambo yanawasumbua ndio maana wanatoa kauli za kudhihaki chombo hicho.




Mhe.
Ndugai amesema hayo jana mjini Dodoma baada ya kuwepo kwa baadhi ya
wabunge wanaotoa kauli zisizokuwa rasmi katika vikao vya bunge bila
kufikiria kwamba wanachokifanya hakina taswira nzuri kwa wapiga kura wao
pamoja na kwa serikali kwa ujumla.

"Yupo
mwenzetu alisimama hapa na kulalamika kuwa bunge hili ni dhaifu, kwa
maoni yangu hizi ni lugha za kuudhi kwa sababu wenzako wengi namna hii
waliochaguliwa na watu wakaletwa hapa halafu wewe unawaona kwa wingi wao
ni dhaifu haipendezi. 




"Unajua
sisi tunaokaa hapa mezani hatuchangii kama nyinyi, kazi yetu ni kuwapa
nafasi  mseme, wakati mwingine zinatoka shutuma ambazo hatuna nafasi ya
kubishana au kulumbana lakini wakati mwingine ni vizuri kutumia fursa
hizi kusafisha baadhi ya mambo. Binadamu ni lazima uwe na staha ile
ndogo tu kuwaheshimu binadamu wenzako,
" alisema Ndungai

Pamoja na hayo, Ndugai ameendelea kwa kusema "Katika
bunge letu kinacholeta matatizo humu ndani ni tabia na lugha,
tukirekebisha hayo mawili tutaenda vizuri tu lakini najua kundi hili ni
kubwa hatuwezi kuwa wote tupo sawa, nitaendelea kulisemea lakini pale
kwenye ulazima tutachukua hatua.
"...Unapomwita kiongozi ni dhaifu, maana yake unamlazimisha awe mkali, achukue hatua. 

"Naona wengine wanahaingaika sijui kufungua kesi....Lakini nasisitiza, Mimi ndio Spika, nasema mwaka mtu hakanyagi hapa"

==>Mtazame hapa Ndugai akifunguka zaidi.
Powered by Blogger.