NYANI AZIMA UMEME KWA MUDA WA ZAIDI YA SAA SITA NCHINI ZAMBIA
Nyani alivuruga mitambo ya umeme katika mji wa Livingstone nchini Zambia na kukata umeme kwa karibu watu 50,000.
Nyani huyo alifanikiwa kuingia katika kituo cha umeme siku ya Jumapili,
na kuvuruga mitambo yenye umeme inayosambaza umeme kuenda maeneo ya
Kusini na magharibi mwa Zambia kwa mujibu wa kampuni ya umeme nchini
humo Zesco.
Alisema kuwa wakaazi 28,000 wa Livingstone na watu wengine 22,000 wa
eneo hilo walibaki kabisa bila umeme kwa zaidi ya saa sita wakati
ukarabati ulikuwa ukiendelea.
"Nyani huyo alipigwa na umeme lakini kutokana na maumbile yake ya
kimazingira alipata tu majeraha mabaya ya moto. Kama angekuwa binadamu
angekufa." alisema Kapata.
Kapata alisema kuwa kampuni hiyo imeomba msamaha wateja wake kwa hasara waliyoipata.
Mji wa Livingstone ni maarugu kwa wanyama pori kama nyani na ndovu wanaotoka mbuga iliyo karibu.