MSICHANA AUAWA, AFUNIKWA MFUKO WA SANDARUSI KISHA KUZIKWA KWENYE SHIMO KISA KAGOMA KUOLEWA RUKWA
NB-Picha haihusiani na habari hapa chini
****
MSICHANA asiyefahamika jina wala umri
wake ameuawa kwa kipigo na kisha mwili wake kufukiwa kwenye shimo huku
ukiwa umewekwa kwenye mfuko wa sandarusi.Mwandishi wa Malunde1
blog,Walter Mguluchuma anaripoti.
Tukio la mauaji ya msichana huyo
lilitokea Julai 18 majira ya saa mbili asubuhi katika kijiji cha Kate
kata ya Kate wilayani Nkasi mkoani Rukwa ambapo uvumi ulienea kijijini
hapo kuwepo kwa mauaji na baada ya uchunguzi ndipo lilipogundulika shimo
na kufukiwa porini umbali wa kilomita moja kutoka kijijini.
Kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa George Kyando alisema baada ya
kulifukua shimo hilo walikuta mwili wa mwanamke huyo na baada ya
uchunguzi wa kidaktari mwili wa marehemu ulikutwa na majeraha matatu
kichwani ya kukatwa na kitu chenye ncha kali kinachodhaniwa kuwa ni
panga.
Kamanda Kyando alidai kuwa marehemu alifika kijijini hapo akitokea
jijini Dar es salaam ambapo inadaiwa ni mwanafunzi na kufika kwa
mwenyeji wake aliyejulikana kwa jina la Samwel Selemani na kumtambulisha
kwa jirani zake kuwa ni mpenzi wake.
"Waliendelea kuishi pamoja baada ya muda kijana huyo alitoweka nyumbani
na kuelekea kusikojulikana na mwanamke mwenyewe hakuonekana na kuwa siku
chache za nyuma kulitokea ugomvi kati mwanaume na marehemu ambapo
mwanamke alikuwa akiomba nauli ya kurudi jijini Dar es salaam kwa madai
kuwa anataka arudi shule lakini mwanaume ambaye ni mtuhumiwa alikataa
kuitoa nauli hiyo akidai kuwa hataki mpenzi wake huyo aondoke",alieleza
Kamanda huyo.
"Baada ya mvutano wa muda mrefu ndipo mtuhumiwa alidai kumuua mapenzi
wake huyo na kuufukia mwili wake kwani hakuwa tayari mwanamke huyo
aondoke kwani yeye alitaka waanze kuishi pamoja wakati mwanamke huyo
alikuwa hayupo tayari kwa madai kuwa ni mwanafunzi.
Marehemu hakuweza kutambulika na kuzikwa eneo la tukio,huku mtuhumiwa
aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wake hajapatikana mpaka hivi sasa na jeshi la
Polisi linaendelea kumtafuta na iwapo atakamatwa afikishwe mbele ya
sheria.
Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blog Nkasi.