MBUNGE MATIKO LAZIMA NIBORESHA MIUNDO MBINU YA ELIMU JIMBO LANGU.






Peter Magwi katibu wa Mbunge Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko akikabidhi Mifuko ya Saruji Diwani wa Kata ya Turwa Zakayo Chacha Wangwe.
Diwani wa kata ya Turwa Zakayo Wangwe akitoa Shukrani zake baada ya kupokea Mifuko ya Saruji kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko.

Esther Matiko ni  Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Kupitia CHADEMA na ni moja ya walioko katika orodha ya watoto wa Kike kutoka jamii ya Wakurya aliyefanikiwa kupata Elimu akiwa mtoto wa Mkulima, Mhe Esther Matiko amesema kuwa ataendelea kuinua Miundombinu ya Elimu ndani ya Jimbo lake.

Ikiwa ni sehemu ya Ilani yake ya uchaguzi ya 2015 - 2020 katika kuhakikisha Jimbo la Tarime Mjini linafanikiwa kuwa na Madarasa ya kutosha, Mhe Esther N. Matiko amewachangia Mifuko 30 ya Saruji wananchi wa Mitaa ya Uwanja wa Ndege na Mkuyuni wanaojenga shule mpya ya Mturu.

Kwa nguvu za Wananchi wa Mitaa hiyo iliyoko Kata ya Turwa wamefanikiwa kujenga Maboma 6 yaliyofika usawa wa Lenta.
Mhe Esther N. Matiko katika kuakikisha ujenzi wa shule hiyo unakamilika mapema ili kuondoa hadha kubwa ya mrundikano wa wanafunzi katika shule ya Msingi Rebu na kusababisha wanafunzi hao kusoma kwa zamu amewachangia wanamitaa hiyo Mifuko 30 itakayotumika kufunga Lenta na kujengea sehemu itakayokuwa imebaki kukamilisha ujenzi wa Maboma hayo.

Mifuko hiyo ya Saruji imekabidhiwa na Katibu wa Mbunge Tarime Mjini Bw Peter Magwi Michael na kuwakikishia wananchi hao kuwa ujenzi wa Maboma hayo yatakapokamilika mapema basi Halmashauri ya Mji wa Tarime nayo itachukua jukumu la Kuezeka Maboma hayo kwa uharaka sana.

Powered by Blogger.