MBUNGE ESTHER MATIKO NITABORESHA MICHEZO TARIME.
![]() |
Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Esther Matiko akikabidhi Seti moja ya Jezi Timu ya Gamasara FC |

Timu ya Gamasara Fc ikikabidhiwa Mpira wa Miguu


Picha ya pamoja na Mbunge wa Jimbo la Tarime mjini Esther Matiko na Gamasara Fc baada ya kukabidhiwa seti moja ya jenzi na Mpira Mmoja
Mbunge wa jimbo la Tarime Mjinikupitia chama cha Demikrasia na Maendeleo CHADEMA Esther Matiko akiwa kama Makamo Mwenyekiti wa Bunge Sport Club na Mwanamichezo wa Bunge aliyefanikiwa kujinyakulia Medali tofauti tofauti katika Mashindano ya Kibunge Afrika Masharikiamesema kuwa michezo kwake ni kipaumbele chake lazima kuahkikisha Tarime anaboresha Michezo.
Mhe Matiko ameipa Jezi Jozi 1 na Mpira 1 Timu ya Mpira ya Gamasara FC inayoshiriki Mashindano ya Ligi Daraja la 4 ngazi ya Wilaya ya Tarime.
Mpaka kufikia wakati wa uzinduzi wa Ligi hiyo Timu ya Mpira ya Gamasara haikuwa na Jezi ambayo wangekutumia katika Mashiindano hayo.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake Nahodha wa Timu hiyo amemshukuru sana Mbunge huyo kwa kuwapatia Mpira na Jezi watakayo itumia katika Michezo hiyio na kumuhaidi Mhe Mbunge kuwa wataibuka Washindi.
Matiko aliitakia kila la kheri Timu ya GamasaraFc katika Mashindano hayo na kuwahidi kushirikiana nao kwa kila hatua ili kuinua Vipawa vya Wachezaji wake.