MBUNGE: MATIKO AMPONGEZA MBUNGE VITI MAALUM SERENGETI CATHERINE.


Kulia
ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA Esther Matiko akiwa na Mbunge wa viti maalum CHADEMA
Wilaya ya Serengeti Mkoani Mara  Catherine Ruge Katika Sherehe ya
kuwashukuru wanachi wa Serengeti pamoja na Mwenyezi Mungu.











Mbunge Matiko akiongea na Wanaserengeti.
Ni ndani ya Wilaya ya Serengeti Mhe Catherine Ruge akitoa shukrani zake za
pekee kwa Mwenyezi Mungu kwa kumuwezesha kuteuliwa na kuwa Mbunge wa Viti
Maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).


Mhe Esther N. Matiko Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini ameweza kuhudhulia Sherehe
hiyo  iliyoambatana na Ibada ya
kumshukuru Mwenyezi Mungu nyumbani kwao na Mhe Catherine Ruge.


Sherehe hiyo iliudhuliwa pia na Naibu Katibu Mkuu Chadema Tanzania Visiwani
(Mhe Salumu Mwalimu) Viongozi wa Chadema Kanda ya Serengeti, Mbunge wa Chadema
Jimbo la Serengeti, Madiwani wa Serengeti pamoja na Madiwani kutoka Tarime
Mjini.


Mh Esther akitoa  wasaa wake kwa wanaserengeti
 ametoa shukrani zake  na kusema kuwa wataendelea kuwatumika
watanzania na wana mmara kwa lengo la kuleta madadiliko.


Itakumbukwa Mhe Catherine Ruge ni zao la Mhe Esther N. Matiko ndani ya
Chadema kwani Mhe Matiko Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Mara ndiye aliyempokea
Mhe Ruge ndani ya Chadema.


Akizungumza mbele ya umati mkubwa uliojitokeza katika Sherehe hiyo Mhe
Matiko amempongeza Mhe Ruge na kumtia Moyo wa ujasili ndani ya siasa na kumsihi
nafasi hiyo apate kuitumia vyema kwa kuwatumikia wanaserengeti, wanamkoa wa
Mara na watanzania kwa ujumla.


Katika kumpongeza Mhe Catherine Ruge, Mhe Esther  Matiko amemzawadia Mhe Ruge Kiwanja cha
kujenga nyumba mkoani Dodoma ili kuwa na Makazi yake katika Kipindi cha Bunge
tofauti na kufikia Hotelini na hata Wanaserengeti watakapomtembelea Bungeni
wawe na Mahala pa kufikia


Kwa heshima kubwa ya familia ya Mhe Catherine Ruge waliweza pia kumshukuru
Mhe Matiko kwa kumkaribisha rasmi ndani ya familia ya Mhe Ruge kwa kumzawadia
Vitenge vya Heshima na Ng'ombe mmoja Jike kama ilivyo tamaduni za Wakurya.


 Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Chadema
(Salum Mwalimu) akiwa ni kiongozi wa chama cha Chadema kutoa Makao makuu
alipata kuhudhulia sherehe hiyo na kuwambia wanamkoa wa Mara kuwa kuteuliwa kwa
Mhe Catherine Ruge kuwa Mbunge wa Viti Maalumu ni heshima kubwa kwa Mkoa wa
Mara na kurudisha fadhila kwa Wanamara walizozitoa katika uchaguzi mkuu wa
2015.


“Itakumbukwa uchaguzi mkuu wa 2015 Mkoa wa Mara ni miongoni mwa Mikoa 3
ambayo Chadema ilifanya vizuri katika uchaguzi huo kwa Mkoa wa Mara kuwa wa 3
baada ya Kilimanjaro na Arusha. 


Mhe Mwalimu aliwaomba sana wanamkoa wa Mara
kuwatumia vyema Wabunge wao wawapo ndani ya Mbunge na hata nje ya Mbunge ili
kutimiza ahadi waliozoahidi katika uchaguzi mkuu wa 2015”alisema Salum.


Mhe Ruge kwa kipekee kabisa alipata kuwashukuru wanaserengeti, Chadema kwa
kumpatia nafasi hiyo na kuahidi kuendelea kuwatumikia kwa uaminifu na uadilifu
wa hali ya juu na kusema kuwa lazima awatumikie vyema kwa lengo la kuletea
wanchi wake maendeleo bila itikadi za vyama.


Mbunge Catherine akimzawadia Kitenge Mh Esther Matiko kwenye  Sherrhe hizo.
TAZAMA CHINI VIDEO  WABUNGE WAKICHEZA NGOMA YA ASILI
Powered by Blogger.