Breaking News: Tundu Lissu Afikishwa Mahakamani
Siku
4 baada ya kukamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
na kuwekwa mahabusu, Rais wa Chama cha Mawakili na Mbunge wa CHADEMA,
Tundu Lissu leo July 24, 2017 amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu akikabiliwa na kesi ya uchochezi.
Tundu
Lissu alikamatwa July 20, 2017 akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere Dar es Salaam akielekea Rwanda kwenye mkutano wa
Mawakili.