Matokeo Kidato cha Sita : Wasichana Waongoza kwa Kufaulu
Matokeo
ya kidato cha sita nchini yalitolewa leo Jumamosi, Julai 15,
yameonyesha kuwa wasichana wameongoza kwa ufaulu ambapo kati ya
wasichana 28,731 (38 asilimia) waliofanya mtihani, waliofaulu ni ni
27,577 (sawa na asilimia 97.21).
Jumla ya watahiniwa 75, 116, walifanya mtihani huo Mei mwaka huu.
Kwa upande wa watahiniwa wavulana, waliofaulu walikuwa ni 42,975 (sawa na asilimia 95.34) kati ya 46,385.
Taarifa
iliyotolea inaonyesha kuwa watahiniwa 58,556 (asilimia 93.72) walipata
daraja la kwanza hadi la tatu. Kati ya hao, wasichana ni 22, 909 na
wavulana ni 35,647.
“Mchanganuo
wa ufaulu katika madaraja unaonyesha kuwa watahiniwa walipata daraja la
1-11 umepanda kwa asilimia 0.59 kutoka asilimia 93.13 mwaka 2016 hadi
93.72 mwaka huu,” imesema taarifa hiyo na kuongeza;
“Pia,
ufaulu katika madaraja kwa upande wa wasichana umepanda ikilinganishwa
na wavulana. Ubora wa ufaulu kwa wasichana ni asilimia 94.07
ikilinganishwa na asilimia 93.49 ya wavulana.”
Ufaulu wa masomo
Kadhalika
taarifa hiyo imeonyesha kuwa ufaulu kwa watanikiwa wa shule kwa upande
wa masomo, ya Sayansi, Biashara, Lugha na Sanaa, haukuonyesha tofauti
kubwa ukilinganisha na mwaka jana.
Hata hivyo, ufaulu katika somo la General Studies umeshuka kwa asilimia 7.54 kutoka asilimia 71. 24 hadi 63.70.