Jamali Malinzi na Mwesigwa mambo Bado Magumu.....Warudishwa Rumande Hadi July 31
Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu
Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamerudishwa rumande kwa
mara nyingine kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika hivyo
wamerudishwa tena Mahakamani Julai 31 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa
tena.
Uamuzi
huo umetolewa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, ambapo
ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea mpaka
sasa.
Malinzi
na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa na matumizi mabaya ya
madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa mahakamani
kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 yakiwemo
kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.