HII NIMECHOMEKEA TU, HUYU NDIYE YULE PAPE NDAW ALIYEACHA GUMZO LA VITUKO VYA USHIRIKINA
Pape Ndaw alikuwa mchezaji mrefu kuliko wote Ligi Kuu Bara, aliitumikia Simba katika kikosi chini ya Kocha Dylan Kerr.
Pamoja na kupewa nafasi mara kadhaa, Ndaw aliishia kuwa kituko na kuzua mjadala likiwemo lile tukio la kukutwa na hirizi katika mechi dhidi ya Prisons huko mjini Mbeya.
Kabla ya hapo, Ndaw aliichezea Simba katika mechi dhidi ya Yanga akiwa na viatu vilivyochakaa kupitia kiasi akadi ilikuwa ni zawadi kutoka kwa bibi yake.
Mshambulizi huyo kutoka Afrika Magharibi, alionekana anaamini ushirikina kupindukia na aliondoka bila kufunga hata bao. Hii nilikuwa nachomekea tu, sijui yuwapi huyu Ndaw wa vituko?