HESLB yavuka lengo, yakusanya bilioni 116
Zoezi
la utafutaji, ufuatiliaji na ukaguzi wa wadaiwa sugu na ambao
wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu mahala pa kazi iliyoendeshwa na
Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kipindi cha mwaka mmoja,
limefanikiwa kwa asilimia 46 na kupelekea makusanyo ya mikopo hiyo
kuvuka lengo lililokusudiwa.
Akiongea
na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, kuhusiana na hali
ya makusanyo ya mikopo kwa wanufaika wa elimu ya juu, Mkurugenzi
Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bwana Abdulrazak Badru
alisema walilenga kukusanya Shilingi Bilioni 76 lakini wamekusanya
Shilingi Bilioni 116 ikiwa ni kiwango cha marejesho cha asilimia 46.
Bwana
Badru alisema, hataacha kutumia mbinu ya ufuatiliaji mahala pa kazi
huku akiwakumbusha wale ambao wanashindwa kurejesha mikopo kwa hiari
sheria itafuata mkondo dhidi yao kwani fedha hizo hutumika kwa wanafunzi
wa awamu mpya ya masomo.
Aidha,
Bwana Badru alitoa onyo kali kwa waajiri ambao wameshindwa kuwasilisha
majina ya waajiriwa wao ndani ya siku 28 kwa bodi hiyo, kuchelewesha
makato baada ya kuwakata waajiriwa ama kuficha taarifa kuwa hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao