Everton Yairarua Timu ya Gor Mahia
Timu
ya Soka ya Uingereza, Everton imewafunga mabingwa wa kombe la SportPesa
2017, Gor Mahia ya Kenya 2-1 katika mchezo ulioshuhudiwa na maelfu
katika uwanja wa Taifa wa Dar es Salaam.
Everton
walikuwa wa kwanza kushindilia goli la kwanza nyavuni kupitia mchezaji
wake mpya Wayne Rooney katika dakika ya 34 akipiga shuti kali umbali wa
takribani hatua 30.
Hata
hivyo, Gor Mahia walifanya purukushani zenye mahesabu mazuri na
kurudisha kipigo hicho ndani ya dakika nne, hali iliyowaweka Everton
mguu sawa. Magoli hayo yalidumu hadi wakati wa mapumziko huku timu hiyo
ya Uingereza ikionekana kumiliki zaidi mpira.
Piga
ni kupige iliyoambatana na makosa ya hapa na pale yaliyokuwa yanafanywa
na Gor Mahia ilipelekea Everton kupata goli la pili lililowekwa nyavuni
na Kieran Dowell aliyewatoka walinzi na kupiga shuti kali, hivyo
kufanya matokeo kuwa 2-1 yakidumu hadi kiliposikika kipyenga cha mwisho.
Tofauti
na wengi walivyotegemea, Gor Mahia walijitahidi kuwapa wakati mgumu
Everton hali iliyosababisha kocha Dylan Kerr kutoa maelekezo ya mara kwa
mara kwa wachezaji wake.
Rooney
pia alikutana na kisiki cha kukamiwa na wachezaji wa Gor Mahia
wakitimiza ahadi yao ya kumdhibiti ingawa nahodha huyo wa zamani wa
Manchester Utd hadhibitiki kirahisi, hali iliyopelekea kuwapa madhara ya
goli moja.