CHANGAMOTO YA MAJI KWA WAKAZI WA SAMINA MJINI GEITA
Hali ya upatikanaji wa maji safi na salama kwa wakazi wa Samina, Kata ya Mtakuja katika Mji wa Geita mkoani Geita bado si ya kurudhisha.
Kumbuka mkoa wa Geita unajulikana kwa kujaaliwa neema ya madini ya dhahabu na hivyo kumfikirisha kila mmoja kwamba huenda miundombinu muhimu katika jamii kama vile barabara, maji, umeme, elimu na afya isingekuwa changamoto tena mkoani humo.
Mmoja wa akina wa mama wa Samina akichota maji kutoka kwenye chanzo cha maji wanachokitegemea huku wengine wakimngojea.
Fuatilia mdahalo kuhusu madini
Picha na Masyenene Damian