Bulaya Ambwaga Tena Wasira Mahakamani
Mahakama
ya Rufani imetupilia mbali rufaa iliyokatwa na wapiga kura wanne wa
Jimbo la Bunda Mjini Mkoani Mwanza ya kupinga ushindi wa Mbunge, Esther
Bulaya katika uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani na Rais wa Tanzania
ulifanyika Oktoba 25 mwaka 2015.
Wapiga
kura hao ambao wanampigania aliyekuwa Waziri wa Chakula, Kilimo na
Ushirika na mgombea ubunge wa CCM Jimbo la Bunda Mjini, Stephen Wasira,
wapo wanne ambao ni; Magambo Masato, Matwiga Matwiga, Janes Ezekiel na
Ascetic Malagila.
Uamuzi huo umetolewa jana na Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Elizabeth Mkwizu ambapo alisema, upande wa walalamikaji uliwasilisha hoja 10 za kupinga ushindi wa Bulaya, lakini hoja hizo hazikuwa na mashiko, hivyo zinatupiliwa mbali.
Miongoni mwa hoja zao ni “Stephen Wassira, hakualikwa katika mchakato wa kujumlisha kura suala hili linaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi kwa kushindwa kumtambua mgombea wala chama chake,”

Baada
ya maamuzi hayo Mbunge huyo kupitia ukurasa wake wa twitter aliandika
maneno machache ambayo alimshukuru Mungu kwa kitendo cha kushinda kesi
hiyo dhidi ya wapiga kura hao.
"Wana bunda wameshinda tena na tena, asante Mungu", aliandika Bulaya.