AUDIO:MTU MMOJA AUWA KWA KUCHOMWA KISU TUMBONI MWINGINE AJINYONGA TARIME

KAMANDA WA POLISI MKOA WA POLISI TARIME- RORYA ACP HENRY MWAIBAMBE
Mtu mmoja
aliyejulikana kwa jina la Murian Manoti  Mkazi wa kijiji cha Msege kata ya Nyarokoba
Wilayani Tarime Mkoani Mara ameuawa  kwa
kuchomwa na Kitu chenye Ncha kali  na Mtu
aliyefaamika kwa jina la Kigumbe Shabani Gibinagwe Mkazi wa kijijini hapo.
Akiongea kwa
njia ya Simu Mtendaji wa kijiji cha Msege Titus Mwera amedhibitisha kutokea kwa
tukio hilo huku akisema kuwa chanzo ni Ugomvi.

Hata hivyo
Kijijini hapo Mtu aliyefaamika kwa jina la
Kaguri Matiko Masongo amejinyonga na  chanzo cha tukio hilo bado hakijafaamika


Diwani wa
kata ya Nyarokoba Matiko Bisendo amelaani vikali kitendo hicho na kusema kuwa
wamekaa na wazee wa mila na kutoa tamko la pamoja kupiga marufuku watu
wanatembea na visu.
Kamanda wa
Polisi Tarime Rorya  ACP Henry Mwaibambe  Amedhibitisha uwepo wa Matukio hayo japo
alikuwa nje ya Ofisi .
HABARI ZAIDI SIKILIZA AUDIO VIONGOZI WANAZUNGUMZIA TUKIO HILO

Powered by Blogger.