YANGA YAANZA KUINGIA HOFU KUHUSIANA NA SIMON MSUVA
Kamati ya usajili ya Klabu ya Yanga inaendelea kukiboresha kikosi chake ambapo leo Jumatano inatarajia kumalizana na kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi ambaye yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, ambacho kinajiandaa kwenda nchini Afrika Kusini.
Kwa muda mrefu Yanga imekuwa ikiifukuzia saini ya kiungo huyo wa Mbeya City kwa ajili ya kumjumuisha kwenye kikosi chake, ambapo sasa habari njema kwao wamefanikiwa kumnasa na itampatia mkataba wa miaka miwili.
Chanzo kutoka ndani ya Yanga, kimesema kuwa viongozi wamepanga kumsanisha kabisa kiungo huyo kabla hajaelekea Afrika Kusini akiwa na Taifa Stars inayokwenda kushiriki michuano ya Cosafa inayosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka Kusini mwa Afrika ambapo kikosi hicho kimealikwa.
“Ishu ni kwamba viongozi wanataka kumalizana na Raphael kabisa kabla hajaenda Afrika Kusini, kesho (leo) Jumatano kuna asilimia kubwa akasaini mkataba wa miaka miwili ya kujiunga na Yanga.
“Usajili wake ni sehemu ya mapendekezo ya kocha George Lwandamina ambaye alitaka asajiliwe kiungo mkabaji ambaye atakuwa na uwezo zaidi ya hawa waliopo kikosini,” kilisema chanzo hicho.
SOURCE: CHAMPIONI