MFUNGAJI BORA LIGI KUU AONYESHA UWEZO WAKE NDONDO CUP...




Usishangae, kwa kuwa straika wa Ruvu Shooting, Abdulrahman Mussa aliyeibuka mfungaji bora kwa msimu huu wikiendi iliyopita aliibukia kwenye michuano ya Ndondo Cup.

Mussa aliyefunga mabao 14 kwenye ligi sawa na kiungo wa Yanga, Simon Msuva aliitumikia timu ya Misosi FC ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi Buguruni Market.

Licha ya uwepo wake uwanjani hapo straika huyo hakufanikiwa kufunga bao lolote kwenye ushindi huo kutokana na mabao yote kufungwa na Idd Seleman ‘Ronaldo’ anayeitumikia timu ya Manispaaa ya Kinondoni (KMC), inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.

Mussa alikuwa sehemu ya wachezaji wanaocheza ligi kuu kuichezea timu hiyo ya Misosi ambapo nyota mwingine ni beki mpya wa Kagera Sugar, Juma Nyosso ambaye amesajiliwa hivi karibuni.
Powered by Blogger.