Picha: Jinsi Shabiki maarufu wa Yanga, Ally Yanga alivyofariki katika ajali ya gari
Shabiki wa Yanga maarufu kwa jina la Ally Yanga amefariki dunia jana katika ajali ya gari. Ally Yanga alijizolea umaarufu mkubwa katika tasnia ya soka kotokana na jinsi alivyokuwa akivaa na kujichora pamoja na namna yake ya ushangiliaji anapokuwa uwanjani.
Ajali hiyo iliyohusika katika kifo cha Ally Yanga iiltokea jana mkoani Dodoma
Klabu ya Yanga kupitia Idara ya Habari na mawasiliano wametuma salamu za rambirambi kwa ndugu na jamaa wa Ally Yanga kufuatia kifo cha mpendwa wao ambapo wamesema kuwa faraja ya Mungu ikawe na familia hiyo katika kipindi hiki kigumu.
“Uongozi wa Yanga SC umepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Ally Yanga, hakika Mungu ni mwema, faraja ya Mungu wetu ikawe kwa familia katika kipindi chote cha majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.”
Aidha, kwa upande wao, Yanga wamesema kuwa wameachwa na pengo kubwa kutokana kutokana na kupoteza shabiki na mwanachama huyo maarufu.
“Pia nasi Yanga kifo chake kina acha pengo kubwa kwa nafasi yake ambayo ilipelekea kujipatia umaarufu mkubwa na alikuwa balozi mzuri kama mwanachama na shabiki mkubwa wa timu yetu, Bwana alitoa, Bwana ametwaa.”