JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA LAPINGA SERIKALI KUFUNGA GAZETI LA MAWIO


Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limepinga kitendo cha serikali kulifungia gazeti la MAWIO na kuahidi kuendelea kupinga vitendo vya uonevu dhidi ya vyombo vya habari ambavyo vinakandamiza uhuru wa habari na kuvunja sheria inayosimamia sekta ya habari nchini.

Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Theophil Makunga ametoa kauli hiyo jana wakati akitoa tamko la jukwaa hilo ambapo amesema, TEF inaushauri uongozi wa gazeti hilo kwenda mahakamani kwa kkuwabwanayo fursa ya kufanya hivyo.

"Kwakuwa chombo ambacho kimepewa mamlaka ya kutoa haki kwa mujibu wa Katiba ya nchi ni mahakama, TEF inauona mlango huo kuwa fursa inayoweza kutumiwa na gazeti la Mawii kutafutavhaki yake kama walivyowahi kufanya wakati gazeti hili lilipofutwa mwaka jana na baadae kurejeshwa na mahakama" amesema Makunga.

Amesema uchambuzi uliofanywa na jukwaa hilo limebaini kuwa kifungu cha 59 cha Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016, kinatoa mamlaka kwa Waziri kuzuia maudhuikatika habari na si kufunguia chombo cha habari.


Makunga amesema kwa kuzingatia uchambuzi waliofanya ni wazi kuwa mchakato ukiotumika kulifungia gazeti hilo umekiuka sheria.
Powered by Blogger.