MWAKALEBELA AREJEA TFF, ACHUKUA FOMU YA KUWANIA KITI CHA JAMAL MALINZI
Frederick Mwakalebela amechukua fomu za kuwania urais wa shirikisho la soka Tanzania (TFF).
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika Agosti 21 mjini Dodoma.
Mwakalebela alikuwa katibu mkuu wa TFF wakati wa uongozi wa Leodeger Tenga.
Baada ya hapo, aliamua kuachana na michezo na kuingia kwenye siasa akigombea jimbo la Iringa mjini kupitia CCM, hata hivyo alikatwa katika kura za maoni.
Alirejea tena katika siasa na kukutana na Peter Msigwa akiwa vizuri, akampiga chini.