Mke mdogo wa Mzee Yusuf Afariki Dunia
Aliyekuwa mfalme wa taarab Alhaj Mzee Yussuf amefiwa na mke wake wa pili (Chiku).
Chiku amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua.
Mzee Yussuf amesema kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana jana saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.