Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk Harrison Mwanyembe amesema serikali itashirikiana na watu
walio tayari kusaidia masuala mbalimbali ya michezo kama ilivyo kampuni
ya michezo ya kubahatisha ya SportPesa.
Dk Mwanyembe amesema uamuzi wa SportPesa
kuanza kwa kusaidia jamii hasa katika michezo, ni jambo
wanalolichukulia kwa uzito au fursa.
“Sisi tutawaunga mkono SportPesa katika
jitihada zao. Lengo lengo ni watusaidie kuendeleza vijana na kupata
akina Mbwana Samatta wengi,” alisema.
“Tunachotaka ni kuwaendeleza zaidi na SportPesa ni kuwaendeleza zaidi,” alisema.
Wakati wa uzinduzi, SportPesa walitoa
kitita cha Sh milioni 50 kusaidia juhudi za Serengeti Boys kufanya
vizuri katika mechi za Kombe la Mataifa Afrika nchini Gabon.
Tayari kampuni ya SportPesa imezinduliwa hapa nchini na imeanza kufanya shughuliz ake.
Kabla kampuni hiyo ilikuwa ikifanya kazi
zake nchini Kenya na imefanikiwa kufanya udhamini katika timu kongwe za
AFC Leopards na Gor Mahia pia Nakuru All Stars.
Kama haitoshi imeeinua Ligi Kuu ya Kenya na sasa imekuwa na umaarufu kutokana na kuwa na udhamini mkubwa.