SPORTPESA WAKAMILISHA WALICHOKISEMA, WAMKABIDHI DK MWAKYEMBE SH MILIONI 50 ZA SERENGETI BOYS
SportPesa ni watu wanaokwenda na
utekelezaji wa ahadi yao baada ya haraka kutimiza ahadi yao ya kutoa
kitita cha Sh milioni 50 kwa kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya
miaka 17, Serengeti Boys.
SportPesa walitoa ahadi hiyo wakati wa
uzinduzi wao juzi na leo wamekabidhi rasmi kwa Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwanyembe.
Abbas Tarimba ambao ni mmoja wa
Wakurugenzi wa SportPesa Tanzania, ndiye alimkabidhi mfano wa hundi hiyo
Dk Mwakyembe leo hii mchana.
Awali Dk Mwakyembe alieleza kufurahishwa
na fursa ya SportPesa na kusema hatailazia damu kwa kuwa angependa
kuona michezo inaungwa mkono.