Wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wakiwa bungeni
wamekubaliana kwa kauli moja kuwa posho za kila mbunge kwa siku ya leo
zipelekwe kwa wazazi wa wanafunzi waliofariki kwa ajali ya basi la Shule
ya awali na Msingi ya Lucky Vincent.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan ameongoza waombolezaji mbalimbali kuaga miili 35 ya marehemu
katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mbali na Makamu wa Rais pia viongozi mbalimbali wa Serikali wameshiriki
zoezi la kuaga miili ya wanafunzi,walimu na dereva waliofariki kwa ajali
Arusha.